
Kuhusu Mafanikio Workshops
Mafanikio Workshops ni programu iliyoanzishwa na kampuni ya Vowels Associates (T) Limited, kampuni inayoshughulisha na utoaji ushauri wa aina mbalimbali kwa watu binafsi na makampuni. www.vowelslimited.co.tz
Tunatumia kanuni zilizoko kwenye biblia kukuwezesha kupata mafanikio unayoyatarajia.
Mafanikio Workshops imejikita kurudisha matumaini kwa mtu aliyekata tamaa na kumuonesha ni namna gani tumeahidiwa kupata kila tunachohitaji kutoka kwa Mungu.
Timu ya Mafanikio Workshops chini ya Mwanzilishi na mkurugenzi wa program hii Ukundi Evans kwa pamoja tunatamani kuona watu wakipata mafanikio yao kama vile wanavyoyatarajia kwa kutumia neno la Mungu.
Kama unatamani kupata mafanikio au kufanikisha malengo yako, hapa ni mahali sahihi kwani utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kupata mafanikio hayo.